Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Stockholm Sweden pamoja na Ubalozi wa Jamnuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Moscow Urusi, tunapenda kuwataarifu wanafunzi wa kitanzania walioko kwenye mji wa Sumy nchini Ukraini kwamba kupitia njia za kidiplomasia , Serikali ya Urusi imeridhia wanafunzi walioko Sumy State University kutoka nchini Ukraini kwa kupitia mpaka wa Urusi.

Zoezi la kutoa wanafunzi wote kutoka Sumy hadi kwenye mpaka wa Urusi litaratibiwa na Serikali ya Urusi na tayari imeanza mipango ya utekelezaji. Wanafunzi hao watakapofika mpakani, Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi utawapokea kwa taratibu zingine za kurejea nyumbani.

Wakati zoezi hili la kuwatoa wanafunzi walioko Sumy likiendelea  kuratibiwa, Balozi zinaomba wanafunzi hao  pamoja na wazazi/walezi kuwa wavumilivu ili kuhakikisha wanatoka kwa usalama nchini Ukraini.

Balozi zetu zitaendelea kuwapa taarifa kila wakati kuhusu utelekelezaji wa mpango huu.

Tunashukuru kwa ushirikiano tunaoendelea kuupata kutoka kwa wanafunzi, wazazi/walezi na Watanzania wote.